MATUKIO

BEYONCE AVUNJA REKODI HII INSTAGRAM

on

Kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness kimetangaza picha ya Instagram iliyovunja rekodi kwa kupata likes nyingi zaidi kuliko picha nyingine yoyote iliyowahi kupostiwa .

Picha ya Beyonce aliyo post juzi  akithibitisha kuhusu ujauzito wake wa Mapacha imeivunja rekodi hiyo kwa kupata likes  milioni 6 (6,335,571) ndani ya saa 8 toka apost ,ambayo hadi sasa ina likes milini 9.5 (9,548,032)

Rekodi  hii ilikuwa ikishikiliwa na mwimbaji Selena Gomez ambae alikua anaishikilia rekodi ya likes Milioni 6 ( 6,305,166 ) kwenye picha aliyoipost June 25 2016. iliyokuwa na caption hii “When your lyrics are on the bottle.”

 

 

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *