KITAIFA

Breaking: Sakata la Makinikia Chadema Wafunguka haya

By

on

DAR: Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umeibuka na kuzungumzia sakata la mchanga wa madini (makinikia) ambalo kwa sasa ndilo linachukua headlines kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

Akizungunmza na wanahabari Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dkt. Vicent Mashinji ameseeleza namna ambavyo chama chao kimekuwa mstari wa mbele kukemea mikataba mibovu ya madini jambo ambalo lilipelekea aliyekuwa mbunge wao, Zitto Kabwe kusimamishwa kuhudhuria bunge mwaka 2017.

Pamoja na hayo, Dkt. Mashinji amekemea kitendo cha wabunge wa chama chake, Ester Bulaya na Halima Mdee kusimamishwa Bunge hadi mwakani kitendo ambacho amesema kinawanyima fursa wabunge hao kuwawakilisha wananchi wao bungeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *