KITAIFA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

on

TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu mapema leo Agosti 11, 2017, ametangaza matokeo ya washindi wa Mashindano ya Taifa ya Afya na usafi wa Mazingira kwa mwaka 2017. Lengo la mashindano hayo ni kuinua hali ya afya na usafi wa mazingira ktk ngazi ya kaya na Taasisi ili kulinda na kuboresha afya ya jamii. 
 
Akitangaza washindi hao katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya, Jijini Dar es Salaam, Waziri Ummy amepongeza wadau mbalimbali kwa kuweza kufanikisha zoezi hilo zikiwemo Halmashauri zote zilizoshiriki. Mashindano haya  yaliweza kushirikisha Halmashauri 185, huku Halmashauri 73 zikishindanishwa Kitaifa baada ya mchujo ngazi ya Mkoa. Mchanganuo wa Halmashauri hizi ni; Majiji – 4, Manispaa 21, Miji 21 na Halmashauri za Wilaya 27.
 
*WASHINDI*
Kwa upande wa Halmashauri za Majiji na Manispaa
1. Manispaa ya Moshi (asilimia 78.5)
2. Halmashauri ya Jiji la Arusha -asilimia 78.1
3. Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Asilimia 67.2.
 
*Halmashauri za Miji*
1. Halmashauri ya Mji wa Njombe (71.9%)
2. Halmashauri ya Mji wa Kahama (71.3%)
3. Halmashauri ya Mji wa Tunduma. (62.1%)
 
*Halmashauri bora inayotekeleza kwa ufanisi kampeni hususani katika ujenzi na matumizi ya vyoo bora*
 
1. Halmashauri ya (W) ya Meru (96.1%)
2. Halmashauri (W) ya Njombe (95.6%)
3. Halmashauri ya (W) ya Makete (80.4.%)
 
*Kijiji bora kinachotekeleza kwa ufanisi usafi*
 
1. Kijiji cha Kanikelele kutoka Halmashauri ya (W) Njombe (95.8%)
2. Kijiji cha Nambala kutoka Halmashauri ya (W) ya Meru (95.3%)
3. Kijiji cha Lyalalo kutoka Halmashauri ya (W) Njombe (93.5%).
 
Vijiji hivi viliweza kupatikana baada ya kushirikisha jumla ya Vijiji na Mitaa 80 huku zaidi ya asilimia 90 ya Kaya zake zikiwa zimefanikiwa kujenga na kutumia vyoo bora pamoja na sehemu za kunawia mikono kwa maji na sabuni.
 
*Hospitali Bora kwa usafi*
1. Arusha Lutheran Medical Centre (96.3%)
2. Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Fransisco, Ifakara – Morogoro (93.6%)
3. Hospitali ya Rufaa Mount Meru, Arusha (89.9%)
 
*Hoteli Bora kwa kiwango cha usafi*
1. Hyatt Regency Dar es Salaam, the Kilimanjaro – 91.1
2. Mount Meru Hotel, Arusha  – 89.0%
3. Aden Palace Mwanza – 87.7%
 
*ZAWADI*
Wizara ya Afya itatoa zawadi ya gari la kubebea taka (trekta lenye tela) kwa Halmashauri ya Mji wa Njombe ambayo imeibuka mshindi wa kwanza kundi la Miji. Na 
Zawadi ya gari mpya aina ya Nissan itatolewa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambayo imeshika nafasi ya kwanza kundi la Halmashauri za Wilaya. Aidha, Zawadi za pikipiki aina ya YAMAHA zitatolewa kwa washindi wote waliosalia ili kutoa motisha kwa mabwana Afya na watendaji wengine walioko katika Halmashauri hizo.
Wizara itaandaa siku maalum kwa ajili ya kukabidhi zawadi hizo. 
 
Aidha Waziri Ummy anawapongeza Viongozi na Watendaji wa Halmashauri zote zilizoshiriki. Tathmini iliyofanywa na Banki ya Dunia mwaka 2012 ilibainisha kwamba Tanzania inapoteza takribani bilioni mia tatu kila mwaka kutokana na hali duni ya usafi. Aidha,  tafiti pia zinaonyesha kuwa kati ya wagonjwa wa nje mia moja wanaoenda hospitali, wagonjwa 60 hadi 80 wanatokana na matatizo ya usafi. 
Waziri Ummy anawahimiza wananchi kuimarisha afya na usafi wa mazingira katika maeneo yao. Usafi ni Wajibu Wetu Sote, alisema.
 
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
11/August 2017

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *