MATUKIO

MACHINGA MBEYA WATUMIA KAULI YA RAIS DK. MAGUFULI KUFANYA BIASHARA KIHOLELA

on

Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashlindi akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Sokomatola (hawapo pichani) Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Zackaria Machoa akifafanua kuhusu utaratibu wa wafanyabiashara kutaka eneo la kufanyia biashara zao badala ya kujiamlia wenyewe Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Sokomatola jijini Mbeya, Abdalah Shaibu akitoa ombi la kuruhusiwa kufanya biashara eneo ambalo wamebomolewa kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sokomatola waliobomolewa vibanda vyao kutokana na kujenga eneo lisiloruhusiwa Baadhi ya Wafanyabiashara wa Sokomatola wakiwa kwenye kikao na uongozi wa Jiji la Mbeya Wafanyabiashara wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuruhusiwa kuendelea kufanya biashara katika eneo ambalo haliruhusiwi Baadhi ya mabanda ambayo yalibomolewa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kutokana na kujengwa katika eneo ambalo haliruhusiwi.

 

WAFANYABIASHARA ndogo ndogo (Machinga) jijini Mbeya wanatumia Kauli ya Rais Dk. Magufuli kufanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Machinga hao wapatao 24 wameamua kujenga vibanda vya Biashara nje ya Soko la Sokomatola kinyume na taratibu huku wakisisitiza kuwa wanafuata Kauli ya Rais kwamba hata ikiwezekana wafunge  Barabara ili wafanye biashara zao.

 

Kutokana na Hali hiyo Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ulibomoa vibanda hivyo hali iliyozua vurugu baina ya Mgambo wa Jiji na Wafanyabiashara hao wakidai waachwe waendelee na biashara licha ya kukiri eneo hilo haliruhusiwi kwa mujibu wa Sheria.

 

Akizungumza katika kikao cha usuluhishi ambacho kiliitishwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Mchungaji David Mwashilindi na kuhudhuriwa na Mbunge wa Mbeya mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi, Mkurugenzib wa Jiji la Mbeya Zakaria Machoa alisema kwa mujibu wa sheria wafanyabiashara wakihitaji eneo la biashara lazima waandike barua ambayo itapita serikali ya Mtaa, Kata kisha Halmashauri.

 

Alisema Wafanyabiashara hao walijiamuria wenyewe bila kufuata taratibu za kuomba kupanua eneo la soko ili waweze kuuzia nje ya Soko kwani hata Ofisi ya Serikali ya Mtaa haikuwa na Taarifa wala Ofisi za Kata pia hazikuwahi kupokea barua za maombi kutoka kwa wafanyabiashara hao.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Sokomatola, Abdalah Shaibu alikiri kuandika barua ya kuomba kupatiwa eneo lakini haikujibiwa hadi hapo Wafanuabiashara walipoamua kuanza kujenga vibanda ili wafanye biashara kutokana na ufinyu wa maeneo na kusisitiza kuwa uamuzi waliochukua ni kuunga mkono kauli ya Rais Dk. Magufuli.

 

Aidha baadhi ya Wafanyabiashara waliobomolewa vibanda vyao walikiri kufanya ujenzi huo kinyume cha taratibu ambapo waliuomba uongozi wa Jiji kutumia busara kuwaruhusu kuendelea kufanya biashara katika eneo hilo hadi utaratibu mwingine utakapotolewa.

 

“Nikuombe Mkurugenzi na Meya tumieni Busara kama ilivyotumika katika masoko mengine kama Kabwe na Mwanjelwa mturuhusu tufanye biashara kule ndani hakutoshi na sisi tupo tayari kulipa ushuru na kufuata taratibu zote” alisema Beth David Mfanyabiashara Sokomatola.

 

Naye Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) alisema msimamo wake tangu 2010 ni kuona kila mwananchi anapewa haki ya kujitafutia riziki hivyo anaungana na wafanyabiashara kumuomba Meya awaruhusu kufanyabiashara eneo hilo kwa masharti ya kuzingatia usafi wa Jiji.

 

“Mimi kama Mbunge nabariki Wafanyabiashara kuendelea na biashara katika eneo hili lakini tuzingatie usafi na maboresho mengine ya kuhamisha au kutafuta eneo lingine tutafuata taratibu za vikao hivyo naomba Mheshimiwa Meya waruhusu watafute riziki wananchi hawa” alisisitiza Sugu.

 

Kwa aupande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi alisema Halmashauri ya Jiji limewaruhusu kufanya biashara eneo hilo kwa muda hadi watakapotafutiwa eneo la kudumu kwani kinachotakiwa ni Halmashauri kuwa na amani na utulivu.

 

Aliongeza kuwa wataendelea kuwepo hapo hadi pale utaraibu wa kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaofanya maeneo ambayo hayaruhusiwi hususani barabarani kwa kuwatafutia maeneo ya kwenda kabla ya kuwaondoa kabisa.

Recommended for you

2 Comments

 1. TangelaZbhik

  February 21, 2017 at 10:03 pm

  I see your page needs some unique content. Writing manually
  is time consuming, but there is solution for this.
  Just search for – Masquro’s strategies

 2. Lauri

  February 22, 2017 at 7:33 am

  Infogalactic and aoso Everipedia arre terrific, however when I googled
  Individual’s Dice recently, Wikipedia was right on top of the initial web page (still showing a cached details in the Dice). http://charlesfilterproj1.com/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *