MATUKIO

Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu, Prof.Sylivia Temu aongoza maadhimisho ya kilele cha siku ya mtoto wa Afrika mkoani Dodoma

By

on

MAADHIMISHO SIKU YA MTOTO  AFRIKA.
 
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Sylivia Temu amewataka Wazazi, walezi na walimu  kuwalea watoto  katika misingi ambayo itawafanya wawe viongozi na hata wazazi bora katika maisha yao ya baadae.
 
Profesa Temu amesema hayo hii leo katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika katika kijiji cha Humekwa, Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
 
Profesa Temu amewasihi Watoto kupenda kusoma na kuacha kujiingiza kwenye makundi ya matumizi ya  dawa za kulevya, na badala yake watoto wajikite zaidi katika kusoma kwa bidii ili wawe  viongozi bora na wenye maadili sahihi katika taifa.
 
Profesa Temu pia amesisitiza tabia ya baadhi ya wazazi wanaowaoza watoto wakiwa katika umri mdogo kuacha tabia hiyo na badala yake wazazi wawe mstari wa mbele katika kuhakikisha Elimu inapewa kipaumbele zaidi kwa mtoto wa kike.
 
Kauli mbiu ya maadhimisho ya  siku ya mtoto wa Afrika ni: Maendeleo Endelevu 2030 " Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto."
 
Picha mbalimbali kutoka kwenye maadhimisho hayo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *