ARUSHA YETU

SASA NI RUKSA KUANDIKA HABARI ZA DC MNYETI.

on

Ndugu waandishi wa habari  wa Mkoa wa Arusha, habarini za Asbh.
Kama kichwa cha Habari kinavyosomeka, hivi Sasa ni ruksa kuandika taarifa za Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.
 
Ni miezi kadhaa imeshapita wakati viongozi wa APC, wajumbe wa kurugenzi  za APC na waandishi waandamizi Mkoani kwetu kufanya kikao cha usuluhishi na DC mnyeti.
 
Hii ilifanyika baada ya DC mnyeti kuomba kufanya hivyo akiamini hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho na hata vitabu vya Mungu vinatueleza kuwa samehe saba mara sabini. Ugomvi siku zote haujengi, kikubwa mtashindana na mmoja iko siku ataumia.
 
 Wajumbe waliohusika walisikiliza pande zote kwa maana ya DC mnyeti na Mwandishi Lihundi, na kubaini uwepo wa mapungufu ambayo kila mmoja alikiri kukosea na kukubaliana kusameheana.
 
Sisi kama waandishi ambao kwa hakika tuliguswa sana baada ya mwenzetu kukamatwa na kuwekwa rumande na pengine lugha isiyokuwa Rafiki kwa baadhi ya wezetu pale walipotaka kufanyakazi wilaya ya Arumeru tunaombwa tusamehe pia, na hivyo tusahau yaliyopita na tugange yaliyo mbele yetu.
 
Dc Mnyeti ni binaadam na ni mkristo safi anayeamini katika kusamehe na pia Lihundi ni mwislam safi anayeamini pia katika kusamehe basi na sisi tusamehe, tuendelee kufanyakazi kwa weledi.
 
Arumeru ni yetu na ina fursa nyingi sana, Dc Mnyeti anawakaribisha waandishi wote kufika Arumeru kwaajili ya Kazi na pengine kupata fursa, na yupo tayari kutoa msaada pale panapowezekana.
 
Tahadhari
 
Kuna baadhi ya maneno yalisambaa kwamba baadhi yetu tuliofanya kikao cha usuluhisi na Dc mnyeti tulihongwa. Haya si maneno mazuri na hayafurahishi kusikia, tunaomba waandishi tusipende kueneza maneno yasiyokuwa na ukweli, kwa kuwa na sisi tulikwazwa na maneno hayo  na kwa kuwa na sisi tunaamini katika kusamehe, tumewasamehe hao walioeneza maneno hayo ambao  wanafahamika na nisingependa kuwaainisha hapa.
 
Kikubwa tuendelee kuonyesha upendo, umoja na ushirikiano pale tunapopatwa na Matatizo au furaha.
 
Asanteni
 
Anaandika Seif Mangwangi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *