ARUSHA YETU

Taarifa kutoka ofisi ya Mbunge jimbo la Arumeru mashariki. 12/08/2017

on

Leo Mhe Mbunge wa Arumeru Joshua Nassar ameendelea na ziara yake jimboni kwake na ilikua zamu ya Kata ya maroroni Kijiji cha Maroroni ambapo Mhe Mbunge alihudhuria harambee ya kuchangia  Rola za maji .
 
Katika ziara hiyo Mh Mbunge alifuatana na 
Katibu ofisi ya Mbunge Julius Ayo
Diwani Kata Imbasey Gadiel Mwanda
Diwani Kata ya seela sing,isi Penzila Pallangyo
Diwani Kata ya Poli Frenk ngoe Mbise Bob kiss
Diwani viti maalumu Kata ya Maroroni Dina Mbise
Diwani viti maalumu Kata ya Imbasen Agness Rambo
Mkt baraza la wazee  Wilaya chadema Mzee kitomary
Mjumbe kamati tendaji Wilaya Mzee Dominic Mungure .
Katika harambee hiyo Mhe mbunge alichangia rola za maji zenye dhamani ya sh 2,500,000/Mkurugenzi wa shule ya HARADALI Mch Severua akachangia sh 1,400,000/ wananchi wa Kijiji cha maroroni wakachangia zaidi ya sh ml 3 hivyo kukamilisha malengo yao ya zoezi hilo la kutatua kero ya Maji.
 
Imetolewa na ofisi ya Mbunge Jimbo la Arumeru Mashariki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *